UKRAINE: MASHAMBULIZI ya ndege zisizo na rubani ‘droni’ za Urusi zimeharibu kituo cha kuzalisha umeme na mafuta kilichopo, Kusini mwa Ukraine, usiku wa kuamkia leo.
Al Jazeera imeripoti kuwa, kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameita mkutano wa dharura mjini Paris leo Jumatatu, Februari 17, 2025, ili kujadili namna ya kuisaidia Ukraine katika kukabiliana na mzozo huo.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Shmyhal, vikosi vya Russia vilitekeleza mashambulizi hayo usiku wa kuamkia leo, wakati joto katika maeneo mengi ya Ukraine linatarajiwa kushuka hadi nyuzijoto saba chini ya sifuri (-7°C).
Shmyhal amesema kupitia mtandao wa Telegram kuwa, “Hili lilifanyika kwa makusudi ili kuwaacha watu bila joto katika halijoto ya chini ya sifuri, na kusababisha janga la kibinadamu.”