Dube, Mayele wawania Mchezaji Bora ASFC

KAMATI ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya uteuzi wa wachezaji watano kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB), iliyotolewa leo Ijumaa imesema kuwa tuzo hiyo haikuwa na majina ya wanaowania, wakati tuzo nyingine za TFF zilipotangazwa wiki iliyopita.

“Hatua hiyo ilitokana na kusubiri mchezo wa Nusu Fainali ya pili ya Kombe la ASFC kati ya Singida Big Stars dhidi ya Yanga uliochezwa Jumapili iliyopita.

“Wachezaji walioteuliwa kuwania tuzo hiyo na majina ya timu zao katika mabano ni Prince Dube na Abdul Sopu (Azam), Bakari Mwamnyeto, Fiston Mayele na Clement Mzize (Yanga),” imesema taarifa hiyo.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa  Kamati ya Tuzo imeteua matukio matatu kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezo wa Kiungwana ‘Fair Play’.

“Matukio hayo mawili yanapatikana kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Yanga, ambapo moja amelifanya Saido Ntibazonkiza na lingine amelifanya Jean Baleke. Tukio la tatu linapatikana mchezo wa Geita dhidi ya Simba ambalo lilifanywa na Pape Sakho wa Simba,” imesema taarifa hiyo..

Habari Zifananazo

Back to top button