EAC yaahidi kushirikiana kibiashara

KENYA : NCHI za Jumuiya ya Afrika Mashariki na AU zimeombwa kudumisha ushirikiano ili kufungua mipaka ya biashara na mafanikio mengine ya kimaendeleo.

Hayo yamesemwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Kenya, William Ruto katika  maadhimisho ya sherehe za jamii ya Waluo zilizowaleta pamoja Waluo kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, jimboni Siaya, Nyanza nchini Kenya.

Wakimpigia debe Raila Odinga anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Museveni amesema taifa la Uganda linaunga mkono azma ya Odinga na kusisitiza kuwa, ushindi wake utaleta manufaa makubwa.

Rais Ruto amesema alifanya mazungumzo na Rais Museveni kabla ya kumuidhinisha Odinga kuwania wadhifa huo, akisema kugombea kwake kupo imara zaidi kutokana na kuwashirikisha viongozi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

SOMA: EAC itumie fursa kongamano la Akili Mnemba

Kulingana na Ruto, Odinga yupo katika nafasi bora ya kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili Afrika ikiwemo vita katika baadhi ya mataifa, kando na uimarishaji mifumo ya kibiashara na utangamano inayohimiza utekelezaji wa biashara huria.

 

Habari Zifananazo

Back to top button