EACOP yafadhili masomo wanafunzi 124 nishati

TABORA: WANAFUNZI 124 wa Kitanzania wamepata ufadhili wa masomo ikiwa ni hatua muhimu katika juhudi za kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi kwa ajili ya sekta ya nishati nchini.

Mpango huo wa ufadhili umewezeshwa na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Ltd na WaASCO ISOAF.

Akizunguma katika hafla ya uzinduzi wa ufadhili huo mkoani Tabora, Mkurugenzi wa WASCO ISOAF, Gary Deason alisema: “Leo tunawekeza katika mustakabali wa baadaye, hatutoi tu ufadhili wa masomo, mpango huu utaimarisha familia, kuboresha maisha, na kuweka msingi wa maendeleo ya baadaye ya taifa”.

Aidha, mpaka sasa  idadi ya wanafunzi waliopata ufadhili wakimasomo, EACOP  imefikia 216, ambapo imeelezwa kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa kutoa elimu ya kiufundi yenye ubora wa hali ya juu, kwa kushirikiana na taasisi kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Ufundi Arusha, na vituo mbalimbali vya VETA.

Zaidi ya vijana 71 Kitanzania wamepata nafasi za mafunzo kwa vitendo ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na China, Afrika Kusini, Umoja wa Falme za Kiarabu, na Ufaransa, kama sehemu ya juhudi za maudhui ya ndani za EACOP.

“Ili kuboresha ubora wa ufundishaji wa kiufundi nchini kote, programu ya kufundisha wakufunzi (Train-the-Trainer) imewafundisha walimu zaidi ya 250. “Tunajivunia kuunga mkono mpango huu wenye faida kubwa na tumejizatiti kutoa mafunzo bora kwa hawa wanufaika,” alisema Dkt Zebedayo Kyomo, Mkuu wa VETA Tabora,” ameongeza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button