Elimu ukatili wa kijinsia yafikia vijana Geita

SHIRIKA la Rafiki Social Development Organisation (Rafiki SDO) limefanikiwa kuwafikia vijana 480 wilayani Geita na kuwandaa kuwa walinzi na mabalozi dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa mabinti balehe.

Mpango huo ni sehemu ya Mradi wa Kuwezesha Mabinti balehe Kuendelea na Masomo (KAGIS) unaotekelezwa na Rafiki SDO  kwa ufadhili wa watu wa Canada (Global Affairs Canada).

Akizungumuza na waandishi wa habari  katika uwanja wa Kasamwa mjini Geita, Meneja Mradi wa Rafiki SDO, Eliud Mtalemwa amesema vijana wamefikiwa kupitia mashindano ya michezo.

Ameeleza mashindano yamehusisha kata 16 za mradi na mitaa 118 wilayani Geita, na kila kata imetoa timu ya vijana 30 kwa ajili ya kushiriki mashindano na kujengewa uwezo wa kupinga vitendo vya ukatili.

“Kwa wingi wao tumeweza kuongea nao, kuwapatia ujumbe wa namna bora ya kuwezesha elimu ya mtoto wa kike sambamba na kupinga ukatili wa kijinsia.

“Kupitia mashindano ya michezo tumeshuhudia ongezeko la taarifa za kuibuliwa vitendo vya ukatili wa kijinsia huku mwamko ukiendelea kuwa juu kwa watoto wa kike kupata elimu shuleni,” amesema.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kasamwa, Victor Bashingwa amekiri kiini cha vitendo vya ukatili kwa mabinti balehe ni vishawishi wanavyopata mtaani ikiwemo kutoka kwa vijana wa bodaboda.

Ameeleza elimu ya kupinga ukatili kupitia mradi wa KAGIS imeamsha morali ya vijana kujiepusha na vitendo vya kuwapa mimba, kuwaachisha masomo na kuwaoa mabinti katika umri mdogo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button