EMF wakosoa marufuku hijab michezoni

PARIS, Ufaransa: WANAFUNZI wa Kiislamu wa Ufaransa (EMF) wamekosoa pendekezo la sheria inayolenga kupiga marufuku hijab michezoni, wakidai hatua hiyo ni ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya Uislamu, na kijinsia.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo kwenye mitandao wake wa X, limesema kuwa sheria hiyo inahatarisha haki za Waislamu, ikizuia fursa zao katika maeneo ya umma.

EMF wamesema kuwa pendekezo hilo linajikita katika mtazamo wa kibaguzi, na linalenga kuhalalisha majadiliano ya umma ambayo yatashajiisha tuhuma dhidi ya Waislamu. Shirika hilo limeeleza kuwa sheria hii ni hatua ya kutenga Waislamu na inachochea uharibifu wa amani katika jamii.

Advertisement

Soma zaidi: Ufaransa kupiga marufuku Abaya

Aidha, EMF limeeleza kuwa pendekezo hili linatengeneza tatizo la bandia kuhusu Uislamu na Waislamu, likijumuisha madai ya kijamii yasiyo na uthibitisho.

Shirika hilo limeonya kuwa hatua hii inaleta madhara kwa kanuni za usawa na inaweza kutengeneza wananchi wa daraja la pili katika jamii.

Kwa upande mwingine, EMF limelaani vikali hatua hii, likieleza kuwa ni sehemu ya uchunguzi wa kisiasa wa miili ya wanawake wa Kiislamu, hatua ambayo linadhani ni hatari na inapingana na haki za msingi za raia.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *