England yagonga hodi kwa Pep Guardiola

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.

KWA mujibu tetesi za usajili Chama cha Soka England kimemuulizia Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, mwenye umri wa miaka 53 kuhusu kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England na anatarajiwa kufanya uamuzi juu ya hatima yake katika wiki zijazo.

Pia mhispania huyo anafikiria kusaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja kubaki City.(Telegraph)

Kocha wa muda wa England, Lee Carsley ameambiwa hatapata kibarua cha kudumu katika timu hiyo. (Sun)

Advertisement

SOMA: United kumuuza Maguire, Madrid wamtaka Saliba

Rais wa klabu ya Barcelona, Joao Laporte anajiandaa kufanya kila linalzowekana kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na Norway, Erling Haaland, 24, mwaka ujao au 2026. (Sport – in Spanish)

Newcastle United inapanga kukubali ofa za kumsajili kiungo wake raia wa Paraguay, Miguel Almiron, 30,  Januari 2025 kama sehemu ya juhudi za kukusanya fedha kwa ajili ya kuwekeza upya katika kikosi chao. (Football Insider)

Liverpool ina nia kusajili beki Loic Bade awe mbadala wa nahodha wake raia wa Uholanzi, Virgil van Dijk, 33.

Hatahivyo, Sevilla haitasikiliza ofa zilizo chini ya pauni milioni 16.7 kumsajili mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mundo Deportivo – in Spanish),

Manchester United imekuwa ikimfuatilia kwa karibu winga wa Crystal Palace, Eberechi Eze, 26.(Football Transfers),

Wakati huo huo, Manchester United inaweza kumsajili tena beki wa kushoto Alvaro Carreras, 21, aliyeondoka Old Trafford kwenda Benfica majira yaliyopita ya kiangazi kwa kipengele cha kumnunua tena kwa pauni milioni16. (Mirror)