United kumuuza Maguire, Madrid wamtaka Saliba

MANCHESTER UNITED iko tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza beki Harry Maguire, 31, mwezi Januari. (Star).

Mshambuliaji wa Norway, Erling Haaland, 24, ameamua juu ya mustakabali wake mbali na Manchester City lakini hatajiunga na Paris St-Germain. (El Nacional – in Spanish).

SOMA: TETESI ZA USAJILI ULAYA

Advertisement

Manchester City wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Ureno Diogo Costa, 25, kutoka Porto kama mbadala wa muda mrefu wa Mbrazil Ederson, 31. (Football Insider).

Beki wa Ufaransa William Saliba, 23, anawindwa na Real Madrid lakini hakuna taarifa za nyota huyo kuondoka Arsenal. (Express).

Chelsea, Tottenham na Liverpool wametuma maskauti kumtazama winga wa Borussia Dortmund, Jamie Gittens katika wiki za hivi karibuni (Bild).