Equity yafungua tawi Ubungo kuwakutanisha wafanyabiashara

DAR ES SALAAM: Benki ya Equity imezindua tawi jipya katika eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, ndani ya jengo la Kituo Kikubwa cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali na kuwapatia huduma za kifedha.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Isabela Maganga, amesema lengo la benki hiyo ni kuwezesha ukuaji wa biashara, kuboresha maisha ya Watanzania na kuchochea maendeleo ya sekta ya biashara kwa kuwasaidia wafanyabiashara wa ngazi zote kukuza mitaji na kupanua masoko yao kimataifa.

“Tawi hili la Ubungo litakuwa mahsusi kwa ajili ya wafanyabiashara kukutana na kufanya mazungumzo ya kibiashara, hasa kutokana na uwepo wake katika kituo kikubwa cha biashara,” amesema Maganga.
Ameongeza kuwa tawi hilo litatoa huduma mbalimbali ikiwemo kuweka na kutoa fedha, huduma za kifedha za kimataifa, huduma za biashara pamoja na usaidizi kwa wateja wa benki hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa benki hiyo, Rogers Mdoe, amesema Equity ni benki ya kikanda inayohudumia zaidi ya nchi sita, na uwepo wa tawi hilo katika kitovu cha biashara utarahisisha wafanyabiashara kufanya mazungumzo na kupanua mitandao ya kibiashara.

“Tunatoa pia nafasi kwa wafanyabiashara kufanya mazungumzo ya kibiashara hapa hapa kituoni,” amesema Mdoe.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Wateja Binafsi na Rejareja, Teresia Mayani, amesema benki hiyo imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuwasikiliza wateja na kusogeza huduma karibu zaidi ili kurahisisha upatikanaji wake.
Uzinduzi wa tawi hilo unatarajiwa kuongeza kasi ya shughuli za biashara katika eneo la Ubungo na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na mataifa mengine.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site