Equity yaja na suluhisho kutunza fedha za wafanyabiashara

DAR ES SALAAM: BENKI ya Equity imezindua rasmi akaunti ya Wezesha itakayowasaidia wafanyabiashara wadogo, wanafunzi, vyama na taasisi pamoja na sekta binafsi kukuza na kulinda mitaji yao.
Uzinduzi wa akaunti hiyo umefanyika leo, Februari 11, 2026, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali, huku kaulimbiu ya uzinduzi huo ni “Kesho Bora Huanza Leo”, na lengo ni kubadilisha maisha na kukuza fursa za uwekezaji wa kifedha, kuwahamasisha Watanzania kuwa na uhuru wa kifedha na kufungua milango ya maendeleo ya kiuchumi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo, wa Kati na Binafsi, Theresia Mayanie, amesema akaunti hiyo inaweza kutumika kama dhamana ya kupata mkopo, na lengo la akaunti hiyo ni kukusanya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kutoa huduma za mikopo, hasa kwa wafanyabiashara, ili waweze kutimiza malengo yao na kuchangia kukuza uchumi wa nchi, pia amesema akaunti hiyo inalenga kuwajengea Watanzania uwezo wa kuwekeza kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

Mayanie ameongeza kuwa akaunti hiyo imezingatia ujumuishi kwa kuwahusisha makundi mbalimbali yakiwemo taasisi za serikali, sekta binafsi, wateja wakubwa, wa kati na wadogo, wanafunzi, vikundi, vijana na watu binafsi, pia amesema Benki ya Equity imeendelea kujipambanua kama benki yenye ubunifu jumuishi, na Akaunti ya Wezesha imeundwa kwa kuzingatia falsafa hiyo.
Aidha, ameeleza kuwa akaunti hiyo inatoa riba ya asilimia 13 kwa mwaka, inayolipwa kila mwezi moja kwa moja kwenye akaunti ya mwekezaji, hivyo kumwezesha kupata mapato ya uhakika kila mwezi. Kiwango cha chini cha uwekezaji ni shilingi 500,000, na uwekezaji huo utadumu kwa miaka mitatu. Baada ya muda huo kukamilika, mwekezaji atarejeshewa mtaji wake wote pamoja na faida.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Equity, Prosper Nambaya, amesema uwekezaji huo unatokana na nidhamu thabiti ya kifedha na usimamizi bora wa mitaji ya benki hiyo, ambapo ameeleza kuwa huduma ya kufungua Akaunti ya Wezesha inapatikana katika matawi yote ya benki hiyo nchini, na kwamba benki hiyo inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kupitia huduma za kifedha.
Naye mmoja wa wateja wa benki hiyo George Kumbuka, ameipongeza Benki ya Equity kwa kuanzisha huduma hiyo, ambapo amesema itawasaidia wananchi kufikia malengo yao ya kifedha na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa.





I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com