Erdogan atangazwa mshindi katika uchaguzi wa marudio Uturuki

Wafuasi wa Recep Tayyip Erdogan walisherehekea hadi usiku baada ya rais wa muda mrefu wa Uturuki kupata miaka mingine mitano madarakani.

Huku takriban kura zote zikiwa zimehesabiwa, Erdogan alipata kura zaidi ya asilimia 52 ya kura katika duru ya pili Jumapili, akimshinda mpinzani wake, Kemal Kilicdaroglu, ambaye alipata asilimia 47.86, kulingana na Baraza Kuu la Uchaguzi.

Matokeo hayo yanatarajiwa kuthibitishwa siku zijazo.

Idadi za kura hiyo zinamuweka Erdogan katika historia huku akiongeza utawala wake wa miaka 20 kwa miaka mitano zaidi.

Amemzidi mwanzilishi wa Jamhuri ya Uturuki, Mustafa Kemal Ataturk aliyeiongoza nchi hiyo kwa miaka 15

Erdogan alionekana nje ya makazi yake huko Uskudar, Istanbul, ambapo aliimba kabla ya kushukuru umati wa watu waliokuwepo eneo hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button