ULAYA : UMOJA WA ULAYA umetoa msaada wa euro milioni 5.4 kwa nchi sita za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati zilizoathiriwa na mafuriko yaliyosababisha vifo vingi.
Taarifa hiyo ilitolewa na ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Chad, ikisema msaada huo utawasaidia watu walioathiriwa na mafuriko katika nchi za Afrika ikiwemo Chad, Niger, Nigeria, Cameroon, Mali, na Burkina Faso.
Msaada umepangwa kama ifuatavyo: Niger itapata euro milioni 1.35, Nigeria euro milioni 1.1, wakati Chad na Mali zitapata euro milioni moja kila moja. Cameroon imetengewa euro 650,000 na Burkina Faso euro 350,000.
Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji (IOM), mvua hizo zimepelekea vifo vya zaidi ya 1,500, zikawaathiri watu milioni nne, huku milioni 1.2 wakilazimika kuyahama makazi yao katika nchi hizi sita, pamoja na Guinea.
SOMA : Mafuriko yaua 30 Nigeria