Fainali? Semeni kingine

DURBAN; PENGINE kama kuna watu watakuwa wana furaha zaidi leo kwa Tanzania, basi watakuwa mashabiki wa Simba baada ya timu yao kufuzu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ndiyo watakuwa na furaha hasa kutokana na kejeli za kwamba timu yao haijawahi kufuzu fainali hizo, hivyo hawana medali. Licha ya mashabiki hao kujitetea kwamba mwaka 1993 walifika fainali michuano hiyo ikiitwa Kombe la CAF, lakini utetezi huo umekuwa ukikataliwa na mashabiki wa kizazi cha sasa kwa madai kuwa hiyo michuano tofauti na kwamba Kombe la CAF sio hilo la shirikisho.

Lakini matokeo ya 0-0 leo mjini Durban Afrika Kusini kati ya Simba na wenyeji wao Stellenbosch FC yanaifanya timu hiyo kutinga fainali kwa jumla ya bao 1-0, baada ya ushindi iliyoupata mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Simba sasa inasubiri mshindi wa RS Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria baadaye leo usiku ili kujua mpinzani wake wa fainali.

Mwaka 2023 Yanga ya Tanzania ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho, ikifungwa nyumbani mabao 2-1 dhidi ya USM Alger ya Algeria, kisha ikaenda kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini, hivyo ikakosa kombe kwa kanuni ya bao la ugenini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button