FIFA yaifungia usajili Chippa United madai ya Abdi Banda

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA) limeifungia klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini kutokana na mzozo wa kifedha na mchezaji wao wa zamani Mtanzania Abdi Banda.

Banda, 28, alijiunga na ‘Chilli Boys’ akitokea Mtibwa Sugar Julai 2022 lakini aliachana na klabu hiyo Agosti mwaka huu baada ya kucheza mechi 17.

Hata hivyo, kulikuwa na masuala ya kuondoka kwake, kwani walishindwa kulipa makubaliano yake, ambayo inasemekana kuwa ni Rand 1.2 milioni sawa na Sh milioni 164.


“Tunataka kuzifahamisha pande zote kwamba marufuku ya kusajili wachezaji wapya kimataifa imetekelezwa na FIFA kuanzia leo,” ilisema taarifa ya mtandao wa Disk Times wa Afrika Kusini ambao wanadai ni sehemu ya waraka uliotumwa na FIFA.

Habari Zifananazo

Back to top button