Fisi 17 wauawa Itilima, wanaowafuga wakamatwa

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi amesema katika operesheni inayoendelea ya kutafuta fisi ambao wamekuwa wakisumbua wananchi ikiwemo kung’ata watoto na kuwaua, fisi 17 wameua katika Wilaya ya Itilima.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa alibainisha kuwa katika operesheni hiyo, wamekamatwa baadhi ya wananchi ambao wamekutwa wanafuga wanyama hao majumbani kwao na kutoa onyo kwa wale wote ambao wanaishi na wanyama hao kinyume cha sheria.
Kihongosi alisema hayo jana wakati akitoa tuzo na zawadi kwa askari polisi ambao walifanya kazi vizuri, tuzo ambazo zilitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillius Wambura.
Aidha, alisema baadhi yao wanadaiwa kutumia wanyama hao katika shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri na kueleza kuwa vitendo hivyo vinachafua taswira ya mkoa huo.
Alisema fisi si chombo cha usafiri, bali ni mnyama ambaye anatakiwa kuishi porini au hifadhini na kubainisha kuwa matukio hayo hayakubaliki na yanatakiwa kukemewa na kila mtu.
“Nitoe onyo kali kwa wale ambao wanamiliki fisi kwa matumizi mbalimbali, tutachukua hatua kali za kisheria kwa wale ambao watabainika, ni kinyume cha sheria kuishi au kufuga fisi, tunawataka wale wote weye hizo tabia kuacha mara moja,” alisema.
Aliongeza: “Hili jambo halipendezi hata kidogo, linauchaufua mkoa wetu, Mkoa wa Simiyu una mambo mengi mazuri, mambo ya kumiliki fisi hayakubaliki hata kidogo, kwanza ni kosa la jinai.”
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa mkoa aliwataka waganga wa tiba asili katika mkoa huo kuisaidia serikali kutoa elimu kwa wananchi ambao wanamiliki wanyama hao kuwaeleza kuwa ni kosa kisheria.
Katika hafla hiyo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Simiyu, Edith Swebe aliwataka askari wa jeshi hilo kufanya kazi kwa kufuata misingi na weledi wakati wakitekeleza majukumu yao.
Kamanda Edith alieleza kuwa askari hao wanatakiwa kutambua kuwa wanaangaliwa na watu wengi wakiwemo wananchi na viongozi mbalimbali, hivyo wanatakiwa kitimiza wajibu wao kisheria.



I will immediately grasp your rss feed as I can’t in finding your email subscription hyperlink or e-newsletter service.
Do you’ve any? Kindly permit me recognise so that I may just subscribe.
Thanks.