Ford yakana kuhusika maandamano Kenya

MAREKANI: Shirika la Ford Foundation, linalotetea haki na demokrasia ulimwenguni, limekanusha tuhuma zinazolihusisha kufadhili maandamano ya kupinga serikali ya Kenya kuhusu Muswada wa Fedha wa 2024.

Katika taarifa yao, Ford Foundation imebainisha kwamba madai hayo ya serikali ya Kenya si ya kweli na kwamba hawajafadhili maandamano yoyote dhidi ya muswada huo.

“Ingawa tunatambua haki ya Wakenya kutetea kwa amani nchi yenye haki na usawa, tunakanusha vikali vitendo au matamshi yoyote yanayohamasisha chuki au unyanyasaji dhidi ya taasisi yoyote, mtu binafsi au jamii yoyote,” imesema taarifa hiyo.

Advertisement

Soma:Maandamano Kenya yaua, yajeruhi

Ford Foundation pia imesisitiza kuwa sera yao ni kutofanya upendeleo wowote katika utoaji wa ruzuku zao.

Uamuzi wa kutoa taarifa hii umejiri baada ya Rais William Ruto wa Kenya kudai kwamba shirika hilo linahusika kufadhili maandamano hayo, na kulitaka shirika hilo kueleza ukweli kuhusu ufadhili huo.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Ruto pia amesema wote waliohusika kuandaa maandamano hayo watakabiliwa na mashtaka ya kisheria.

Ford Foundation, iliyoundwa mwaka 1963 na Edsel Ford, mtoto wa mwanzilishi wa Kampuni ya Magari ya Ford, Henry Ford, imejitolea kusimamia haki za watu na maadili ya demokrasia.

Chanzo:BBC