Maandamano Kenya yaua, yajeruhi

KENYA; Zaidi ya watu 30 wamejeruhiwa na mtu mmoja amefariki dunia katika maandamano nchini Kenya ya kupinga mapendekezo ya nyongeza ya ushuru.

Kwa mujibu wa madaktari wamesema mtu huyo aliyepoteza maisha alipata jeraha la risasi mguuni na kuvuja damu nyingi, jambo lililosababisha kupoteza maisha.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/vijana-waandamana-kenya-muswada-sheria-ya-kodi/

Advertisement

Hatahivyo Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema kuwa watu wanane kati ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mbaya. Katika maandamano haya mamia ya watu wamekamatwa na vyombo vya usalama katika miji kadhaa nchini Kenya.

Waandamanaji hao wanaendelea kupinga nyongeza ya ushuru katika mswada tata wa fedha, ambao ulisomwa kwa mara ya pili katika bunge la Kenya.

Mpaka sasa bado wananchi wa Kenya wanaendelea kuhoji kuhusu nyongeza hiyo ya ushuru, ambao unaweza kuathiri ukuaji uchumi wa Kenya kuzorotesha maisha ya wananchi wa Kenya.

Kufuatia ulipuaji wa risasi katika maandamano hayo, mamlaka huru ya kusimamia shughuli za polisi nchini Kenya IPOA, imesema itafanya uchunguzi kuhusu ufyatuaji risasi wakati wa maandamano hayo.