Fountain Gate 3-2 Coastal Union

Sehemu ya wachezaji wa Fountain Gate wakishangalia wakati wa mchezo dhidi ya Coastal Union leo Desemba 13, 2024.

WANABABATI klabu ya Fountain Gate leo imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuichapa Coastal Union kwa mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mabao ya Fountain Gate katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Tanzanite Kwaraa ni Elie Mkono katika dakika 16, William Edgar dakika 47 na Nicholas Gyan aliyefunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 54.

Advertisement

SOMA: Nyuki kung’ata au ni Azam kulamba asali leo?

Coastal Union ilipata mabao yake kupitia Lucas Kikoti aliyefunga kwa penalti dakika ya 44 na Maabad Maulid aliyefunga bao la pili dakika 79.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu unaoendelea sasa kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ni kati ya wenyeji Tabora United na Azam.