Fountain Gate kujinoa ligi kuu

Timu ya Fountain GATE FC ambayo iko katika nafasi ya 8 kwa alama 25 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara iko katika maandalizi ya kupambana na KMC katika mechi inayofutata.
Kocha wa Timu ya Fountain Gate, Robert Matano amesema timu hiyo inaendelea kujinoa vyema ili kuwa bora zaidi kwenye mechi zitakazofuata huku akiwataka wachezaji wa klabu hiyo kuendelea kuwa na moyo wa kuipenda timu yao.
Matano ameyazungumza hayo 28 February 2025 mbele ya waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Wilaya ya Babati, mkoani Manyara wakati wa timu hiyo ilipokuwa ikijikita katika mazoezi ya viungo.
“Nafarijika.sana kuwa kocha wa timu hii ambayo vijana wanajifunza kwa haraka na kufuata ninavyofundisha hope watagain na kupata ushindi ”
Amesema ubora wa timu unatokana na wachezaji kuwa imara wakati wote na hivyo wanapaswa kuchukulia kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni kazi kama zilivo kazi nyingine na jamii isijenge kuwa mchezo huo ni kwaajili ya burudani pekee.
“So tumefanya a lot of educations na lot of training,na pia tumewatengeneza wawe katika hali nzuri ya kufikiria aandaa kuwa na uwezo wa kufikiria,na pia tumefundisha kwa timu kupenda ile kitu unayofanya,kama mchezaji ajielewe yeye ni mchezaji ambao pia kidogo ilikua shida,kwaio wajue football ni kazi”Matano amesema
Afisa Habari wa Klabu ya Fountain Gate ,Issa Liponda maarufu kama “Mbuzi”amesema katika mzunguko wa pili timu hiyo imekuwa na mabadiliko makubwa kuanzia katika benchi la ufundi huku pia wachezaji kuingia kwenye dirisha dogo.
“Michezo inavozidi kukatika ndivyo ugumu wa ligi yenyewe ndivo unavoongezeka kikubwa zaidi,aah sisi tumesisitiza kwenye kuungana na kuwa kitu kimoja na kutopoteza fokasi na kuwa kwenye malengo, kwa Sasa ligi ilivo ukipoteza mchezo mmoja mwenzako akifunga unajikuta upo chini kwahiyo lazima tupambane,” amesema Mbuzi.
Kwa timu yake kumefanyika mabadiliko katika benchi la ufundi na usajili wa wachezaji wengi katika dirisha dogo kumechangia kutofanya vizuri katika mechi zilizopita.
Kwa mujibu wake kuna nuru na mwanga wa kufanya vizuri katika mechi zijazo mpaka mechi zitakapomalizika.
Aidha,Salum Kihimbwa ambaye ni mchezaji mzoefu ndani ya Timu ya Fountain Gate ametoa ahadi kwa mashabiki kuwa wataongeza jitihada kwa mechi 9 zilizobaki kufanya vizuri ili kupata matokeo mazuri.
“Tunawaahidi mashabiki wetu,tunawaomba radhi kwa kilichotokea dulu la pili kwasababu tumebakisha mechi takribani 9,naahidi tutapambana na tutakuepo kama tulivokua dulu la kwanza ilimradi tuiweke timu katika hali nzuri na hali salama”. Kihimbwa amesema
Amesema,yeye kama mchezaji anafanya kila jitihada kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri na kusisitiza kuwa timu yao inapaswa kuwa na utulivu ili kuinusuru kwenye michuano inayokuja.


