LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Katika mchezo huo maafande wa Tanzania Prisons wataikaribisha Fountain Gate.
SOMA: Fountain Gate kuendeleza ubabe Ligi Kuu leo?
Ushindi kwa Fountain Gate kutaipeleka timu hiyo juu ya msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 16 mbele ya Singida Black Stars yenye pointi 13 baada ya michezo 5.
Fountain Gate inashika nafasi ya 2 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 6 ikishinda 4, kupotea 1 na sare 1.
Prisons ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 4 baada ya michezo 5, haijashinda mchezo, imepoteza 1 na sare 4.