LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa Manyara.
Wenyeji Fountain Gate itaialika Kagera Sugar kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati.
SOMA: Kagera vs KenGold: Kipute cha waliohoi Ligi Kuu
Fountain Gate ipo nafasi ya 2 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 10 baada ya michezo 5.
Nayo Kagera Sugar baada ya michezo 5 inashika nafasi ya 13 ikikusanya pointi 4.
Katika michezo mitano iliyopita Fountain Gate imeshinda michezo 3 wakati Kagera Sugar imeshinda mechi 1.