Kagera vs KenGold: Kipute cha waliohoi Ligi Kuu
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendeleo leo kwa michezo miwili kufanyika Kagera na Tabora.
Wageni wa ligi hiyo, KenGold ya Mbeya baada ya kupoteza michezo 3 mfululizo itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
SOMA: Kivumbi ‘derby’ ya majiji Ligi Kuu leo
KenGold ipo nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa Ligi Kuu na haina pointi wakati Kagera Sugar ambayo nayo inasuasua inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo 4.
Kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, wenyeji Tabora United itakuwa mwenyeji wa Fountain Gate.
Tabora United inashika nafasi ya 4 ikiwa na pointi 7 baada ya michezo 4 wakati Fountain Gate ipo nafasi ya 3 pia ikiwa na pointi 7.