‘Fursa bandari Dar itachochea kukuza uchumi’
DAR ES SALAAM; Serikali imesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam utaiwezesha Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuongeza mapato yanayotokana na bandari kutoka asilimia 40 hadi asilimia 67.
Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini.
“Uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kupitia DP World utawezesha TRA kuongeza mapato yanayotokana na Bandari kutoka 40% – 67%.
“Tanzania inapakana na nchi nane ambazo tukitumia fursa hii ya kuwa na Bandari ya Dar es Salaam itachochea kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi,” amesema Matinyi.