Fursa za aina yake zajadiliwa Tanzania na Romania

DAR ES SAALAM: Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania na Romania wamekubaliana kuongeza wigo wa ufadhili wa masomo hususani katika fani za udaktari na ufamasia ambapo Romania imekubali kutoa nafasi kumi (10) za masomo kwa wanafunziwa Tanzania.

Rais Samia, akizungumza na waandishi wa habari  Novemba 17, 2023 amesema Serikali za mataifa hayo mawili  zimezungumzia fursa zilizopo katika sekta za afya na utengenezaji wa dawa,kubadilishana uzoefu katika sekta ya kilimo ikiwemo usindikaji wa mazao na kukabiliana na majanga.

Wakati huo huo, Tanzania nayo imetoa nafasi tano za ufadhili kwa vijana wa Romania kuja kusoma kwenye vyuo watakavyovichagua ikiwa ni fursa ya kuchangia jitihada za Serikali za kujengea uwezo, rasilimali watu na kuimarisha huduma katika sekta mbalimbali.

Akizungumzia mkutano wa mabadiliko ya Tabianchi wa COP28, 2023 Rais Samia amesema Tanzania inatarajia kuweka nguvu suala la nishati na nishati safi ya kupikia, hivyo amemuomba Rais Iohannis kuiunga mkono Tanzania.

Rais Iohannis yupo nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku nne yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya nchi yake na Tanzania uliodumu kwa miaka 62 na ikiwa ni ziara ya kwanza kwa Mkuu wa Nchi kutoka Jamhuri ya Romania kutembelea nchini.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
15 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions….
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Last edited 15 days ago by Angila
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x