Gabon: Jen.Oligui Nguema atangaza kugombea urais

LIBREAVILLE, GABON : KIONGOZI wa kijeshi wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema, ametangaza rasmi azma yake ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Oligui aliahidi awali kukabidhi madaraka kwa raia baada ya kipindi cha mpito kufuatia mapinduzi yaliyomuondoa Rais Ali Bongo Ondimba kutoka madarakani mnamo Agosti 2023.

Hivi karibuni, Bunge la Gabon lilipitisha sheria mpya ya uchaguzi, ambayo ilifungua njia kwa wanajeshi na mahakimu kushiriki katika uchaguzi.

Katika hotuba aliyotoa Jumatatu kwenye mji mkuu wa Libreville, Oligui alisema kuwa baada ya kutafakari kwa kina na kujibu maombi kutoka kwa wananchi, ameamua kugombea nafasi ya urais.

Akielezea maono yake, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 50 alieleza kuwa anatarajia muhula wa miaka saba utakaohusisha mabadiliko makubwa na maendeleo kwa Gabon.

Alisisitiza kuwa kipaumbele chake kitakuwa ni kuboresha miundombinu ya nchi na kuleta ustawi kwa wananchi wake. SOMA:ECOWAS yatangaza muundo mpya wa majadilino kwa nchi zilizojiondoa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button