KENYA : ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua ameondolewa haki ya ulinzi na usalama.
Akithibitisha hilo, Gachagua amesema lolote likimpata basi Rais William Ruto atawajibika na kadhia hiyo.
Gachagua bado ameendelea kusisitiza mashtaka aliyofunguliwa yalichochewa na masuala ya kisiasa dhidi yake.
Naye Msemaji wa Polisi nchini Kenya Resila Onyango amesema taarifa ya kuondolewa haki ya ulinzi na usalama kwa aliyekuwa Makamu wa Rais Gachagua hana taarifa lakini atalifanyia uchunguzi zaidi.
Hivi karibuni, Bunge la seneti nchini Kenya lilimvua madaraka ya umakamu wa rais baada ya kujiridhisha amekiuka sheria za uongozi.