Rigath Gachagua awahishwa hospitali

NAIBU Rais wa Kenya, Rigath Gachagua amewahishwa hospitali mara baada ya kuumwa gafla wakati Bunge la Seneti likitarajia kusikiliza kesi yake ya kuondolewa madarakani.

Gachagua alitarajiwa kutoa ushahidi leo kuhusiana na shutuma zilizotolewa dhidi yake na Bunge la Kenya. Taarifa ya kiongozi huyo kuwahishwa hospitali imetolewa na Wakili Mkuu, Paul Muite.

Kufuatiwa taarifa hiyo, Spika wa Bunge ameahirisha uamuzi wa kusikiliza utetezi wa kiongozi huyo mpaka hapo baadaye.

Advertisement