Gamondi: Wanaojiuliza maswali watapata majibu
KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anaridhishwa na kiwango cha wachezaji wake inagawa kuna nyakati mambo hayaendi sawa lakini haangalii mchezaji mmoja mmoja bali zaidi matokeo ya timu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Pamba Jiji Dar es Salaam Oktoba 3 Gamondi amesema mchezaji kuwa na siku mbaya kazini ni kawaida duniani kote hata kwa wachezaji wakubwa Ulaya.
Amejigamba kwamba hana wasiwasi kabisa na timu yake.
SOMA: Yanga kama hawapo vile!
“Kama unajua mpira huwezi kuwa na mashaka na Yanga. Nafikiri wale ambao wanajiuliza uliza maswali watapata majibu, muda utaongea,” amesema Gamondi.
Amesema kuna muda wachezaji wanaweza kufunga goli moja au wasifunge kabisa na kwamba kitu ambacho hawezi kuahidi, ni idadi ya magoli.
Ameongeza: “Nachoweza kuwaambia mashabiki ni kwamba tuna uhakika wa kujitoa na kucheza vizuri. Hii ni ligi, tuna mechi 30, tumeshacheza mechi 3 tuna alama 9, na tuna furaha.”
Kocha Msadizi wa Pamba Jiji Henry Mkanwa amesema timu yake imejiAndaa kwa ajili ya mchezo huo.
“Vijana wangu, benchi la ufundi tuko tayari kupambana na anga lakini hatuna presha na lolote linawezakana,” amesema Mkanwa.