Gavana, Katibu Mkuu Hazina waapishwa
Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan leo Januari 9, 2023 amewaapisha viongozi watatu amemuapisha Dk Natu El-Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.
Rais Dk Samia amemuapisha Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Emmanuel Mpawe Tutuba ameapishwa kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, hafla hiyo imefanyika katika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dk Natu El-Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Griffin Venance Mwakapeje na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Mpawe Tutuba wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.
Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais, Dk Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Mpogole Kusiluka, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dk Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Griffin Venance Mwakapeje na Kamishna wa Maadili, Jaji Sivangilwa Mwangesi mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.