MAREKANI : SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi wa Kipalestina la UNRWA, limetoa tathmini yake kuhusu hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Tathmini hiyo inaonyesha kuwa ukanda wa Gaza kuna idadi kubwa ya watoto waliokatwa viungo ukilinganisha na maeneo mengine duniani.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anthony Guterres amesema, “hali iliyokuwepo katika ukanda wa Gaza inatisha na vinavyoendelea kufanyika ni uhalifu wa kimataifa”, alisema Guterres.
Aidha amesema watu waliokimbia makazi yao huko ukanda wa Gaza wako katika hatari ya kukabiliwa na hali ya hewa ya baridi na mvua katika msimu huu wa baridi.
UNRWA imelazimika kusitisha uwasilishaji wa misaada tangu Desemba 1 kupitia kivuko cha mpaka cha Karem Abu Salem – mahali pa kuingizia misaada ya kibinadamu katika eneo la Palestina.
Watu zaidi ya milioni 1 huko Gaza wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi ya Israel na amri za kijeshi, na wengi wao wameyakimbia makazi yao.
Wafanyakazi wa shirika la UNRWA pia ni miongoni mwa waliouawa tangu kuanza kwa vita vya Israel dhidi ya Hamas Oktoba 7, 2023. SOMA : Viongozi G20 wataka kusitisha mapigano Gaza
Hadi sasa kuna vituo saba tu kati ya 27 vya UNRWA vinavyofanya kazi na kutoa huduma za kibinadamu katika eneo hilo la ukanda wa Gaza..