GGML kutumia michezo kuimarisha utendaji kazi

GEITA:KAMPUNI ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu ya Geita (GGML) imetambulisha tamasha la michezo kwa watumishi litakalofanyika kila baada ya miezi mitatu ili kuimarisha utendaji na mahusiano kazini.
Kaimu Mkurugenzi wa Raslimali Watu GGML, Dominick Marandu ametoa taarifa hiyo katika uzinduzi wa tamasha kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya wasichana Nyankumbu Geita.

Amesema tamasha hilo litafahamika kwa jina la Geita Sports Club Bonanza linalenga kuwawezesha watumishi kupata nafasi ya kujumuika, kufurahi na kufanya mazoezi ya afya mwili na akili.
“Tunafahamu michezo ni afya, lengo si kushindana bali ni kuimarisha afya na mahusiano hivo ni jambo ambalo tumelianza sasa na litakuwa endelevu kila baada ya miezi mitatu” amesema.

Amesema, dhamira ni kuwaleta pamoja wadau, wafanyakazi, wakandarasi na kujenga mahusiano baina ya GGML, taaasisi na kampuni tofauti kutoka ndani na nje ya Manispaa ya Geita.
Mwenyekiti wa GGML Sports Club, Valence Ibrahimu amesema Geita Sports Club Bonanza imekuja ikiwa ni maazimio ya wafanyakazi na viongozi matarajio ikiwa ni kuleta matokeo chanya kazini.

Amesema bonanza hilo la michezo litafanyika mara nne kwa mwaka ili kuimarisha mahusiano mahala pa kazi pamoja na afya ya mwili na akili kwa watumishi wa Idara tofauti ndani ya GGML.
“Kila robo mwaka tutakuwa tunafanya mara moja, kwa kuanza tumeshirikisha watumishi kutoka wakandarasi wa kampuni tofauti zilizopo GGML na wengine kutoka Manispaa ya Geita”, amesema.

Katibu Msaidizi wa GGML Sports Club, Irene Mfwele amesema tamasha limezinduliwa kwa michezo tofauti ikiwemo mbio ndefu na mbio fupi, mpira wa miguu, mpira wa pete na kikapu.

“Tamasha hili limekutanisha wafanyakazi wa Idara na kampuni tofauti, imetusaidia kujenga mahusiano kati ya kampuni moja na nyingine, na mahusiano baina ya mtu na mtu.

“Kampuni ina watu wengi hivo siyo rahisi kuonana na kukutana, lakini kwa tamasha hili limeweza kutukutanisha pamoja kwa ajili ya kushauriana na kutengeneza urafiki”, amesema Irene


I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. www.join.work27.com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com