Gidion jela kwa kumkata Thomas vidole

MAHAKAMA ya Wilaya ya Iramba imemuhukumu Gidion Soza ,22, mkazi wa kijiji cha Mingela-Shelui, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, kifungo cha kwenda jela miaka mitano na kupia faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kumjeruhi Thomas Shamsua ,25, kwa kumkata vidole vya mkono wa kulia kwa kutumia kisu.
Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Singida, ambapo imesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mingela, ambapo Gidion alikamatwa na Jeshi la Polisi mnamo Septemba 14, 2024, katika kijiji cha Nsusu na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iramba kujibu tuhuma zilizokuwa zinamkabili, ambapo alikana mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.
Aidha Mahakama ilimuhukumu Gidion kufungwa jela kwa miaka mitano na kulipa fidia ya Shilingi 500,000 kwa muathirika Thomas Shamsua. Hukumu hiyo imetolewa kama tahadhari kwa watu wengine wenye tabia ya kufanya vitendo vya ukatili kama hivyo.
Kwa upande wa familia ya muathirika, wameonyesha kuridhishwa na hukumu hiyo na kusema itakuwa fundisho kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili na umuhimu wa kujizuia kufanya vitendo vya aina hiyo.
lia kwa kutumia kisu.
Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Singida, ambapo imesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mingela, ambapo Gidion alikamatwa na Jeshi la Polisi mnamo Septemba 14, 2024, katika kijiji cha Nsusu na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iramba kwa ajili ya kujibu tuhuma zilizokuwa zinamkabili, ambapo alikana mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.