Gigy aamua kuokoka

MSANII wa Bongo fleva Gift Stanford ‘Gigy Money ameamua kuokoka na kufuata nyayo za msanii mwenzake Irene Uwoya ambaye kwa sasa ni Mama Mchungaji na kutangaza rasmi kuwa Friend of God kutangaza Mungu.

Gigy Money ameandika kuwa upendo wa Mungu juu yake ni mkubwa na ameuona ukuu wake anampenda na akuahidi kutangaza Mungu.

“Kama ni upendo wa Mungu Juu yangu umenionesha ukuu wake Nakupenda Sanaa… na nitamtangaza Mungu na ukuu wake kuonyesha makopa Ahsante sana Tinny Irene Uwoya sasa Mimi (now am) Friends of God Nakupenda Irene na yote tulio ongea yote naahidi kuyafanyia kazi Amen.”ameandika Gigy Money

Advertisement

Naye Mama Mchungaji Irene Uwoya alijibu kwa kuandika,”Amen mama Mungu akutangulie na roho Mtakatifu akusaidie ufanye kusudi la Mungu nakupenda “