Gwajima: Wanawake Wajasiriamali tumieni mitandao
ARUSHA: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima amewataka wanawake wajasirimali nchini kutumia mitandao ya kijamii kwaaajili ya kutangaza bidhaa wanazozalisha ili kupata masoko ndani na nje ya nchi.
Dk Gwajima ameyasema hayo wakati wa kukagua mabanda ya maonesho yaliyoandaliwa na wanawake mbalimbali kwaajili ya maadhimisho ya Siku ya Mwanamke anayeishi kijijini yaliyofanyika Kijiji cha Olevolos, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha yenye kauli mbiu isemayo “Wezesha Wanawake Wanaoishi Kijijni Kwa Uhakika wa Chakula ,Lishe na Uendelevu wa Familia”
Amesema endapo watafungua akaunti kupitia mitandao ya kijamii wataweza kupata masoko kwaajili ya kuuza bidhaa zao wanazozalisha zinazotokana na ubunifu wanaofanya na kuunganishwa na masoko ndani ya nchi na nje.
Amesisitiza wanawake kuendelea kuzalisha zaidi chakula ili kuhakikisha lishe zinapatikana ndani ya familia ingawa wanawake wanaonewa na mwaka jana zaidi ya ukatili wa kijinsia kati 12,000 watoto 10,000 ni wakike,1500 wanalawitiwa na kinababa jiulizeni kwanini mnafanyia ukatili watoto wa kike na mnalawiti watoto wakiume.