Dk . Samia kulinda haki za watanzania

KAGERA : WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro, amesema upendo wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haujaishia kwenye maendeleo pekee bali pia katika kuhakikisha wananchi wanapata haki zao.
Akizungumza mkoani Kagera, Dk. Ndumbaro alisema kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria, Rais Samia anahakikisha kila Mtanzania anafahamu na kupata haki yake.

Alisisitiza kuwa Ibara ya 13 ya Katiba inatamka kuwa binadamu wote ni sawa mbele ya sheria, hivyo huduma za msaada wa kisheria hutolewa bila malipo kwa watu wa makundi yote.
Katika ziara hiyo, Dk. Ndumbaro alikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Shule ya Msingi Igayaza katika Halmashauri ya Karagwe na Mradi wa Maji wa Nyabiyonza.
SOMA: ‘Sheria Huduma za Habari haijatoa huruma kwa wasio na sifa’



