Serikali yaombwa kurejesha mfumo mizigo kidogo kidogo

DAR ES SALAAM:CHAMA Cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) na Chama Cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) wameiomba serikali kurejesha mfumo wa kutoa mizigo kidogo kidogo ili kusaidia kupunguza gharama kwa wafanyabiashara.

Hayo ameyasema leo Aprili 24 na Mwenyekiti wa Chama Cha Mawakala Wa Forodha Tanzania(TAFFA), Edward Urio na kuongeza kuwa kurejeshwa kwa mfumo huo kutasaidi kurejesha thamani ya mnyororo wa thamani.
“TATO na TAFFA tunaiomba Serikali kushughulikia na kurekebisha hali hii utekelezaji wa sheria zilizopo pamoja na mabaresho ya mfumo ya utoji mizigo ikiwemo kuruhusu utoaji wa mizigo kidogo partial release ni hatua muhimu zitakazosaidia kupunguza gharama zisizo na ulazima na kuongeza ufanisi katika mnyororo wa ugavi,”amesema Urio.

Kwa Upande wak,e Elias Lukumay Mwenyekiti wa Cha Cha Mawakala Wa Forodha Tanzania (TAFFA) amesema bandari kwa sasa imeongeza ufanisi katika utoaji wa Huduma zake hivyo changamoto hiyo ikitatuliwa itasaidia zaidi kiutendaji kazi.



