‘Hakikisheni taasisi za fedha zinakidhi vigezo Mpanda’

MKUU wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Jamila Yusuf,  amemtaka ofisa biashara na wadau wengine wanaosimamia sheria za uanzishwaji wa taasisi za kifedha kuhakikisha taasisi hizo zinafuata sheria na kukidhi vigezo vya kuanzishwa kwake Manispaa ya Mpanda.

Jamila ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichokaa kwa lengo la  kujadili rasimu  ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema kutokana na malalamiko ya wananchi, anasubiri kupelekewa orodha na taarifa sahihi kuhusu taasisi hizo, ili aweze kuchukua hatua ikiwemo kuzifuta au kuzihamisha katika wilaya hiyo.

 

Baraza hilo la Madiwani limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya shilingi billioni 26.4 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Ofisa Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji katika Manispaa ya Mpanda, Leonard Kilamuhama, amesema halmashauri imejipanga kikamilifu kuhakikisha wanafuatilia mapato katika maeneo yote yaliyopangwa.

Ametaja maeneo ambayo yatapewa kipaumbele ni pamoja na ujenzi wa maboma 100 ya madarasa sambamba na kulipa posho za wenyeviti wa vijiji na kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii.

Habari Zifananazo

Back to top button