ASIA : IDADI ya waliofariki kutokana na Kimbunga Yagi nchini Myanmar imefikia watu 293, huku wengine 89 wakiwa hawajulikani walipo.
Hayo yameelezwa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya kusini mwa Asia, huku vyombo vya habari vikiripoti kuwa msaada wa kwanza wa kigeni umeanza kuwasili nchini humo.
Zaidi ya ekari 660,000 za mpunga na mazao mengine ziliharibiwa na mafuriko huku wanyama zaidi ya 100,000 wakifariki.
Kimbunga Yagi kiliyapiga maeneo ya Kaskazini mwa mataifa ya Vietnam, Laos, Thailand na Myanmar zaidi ya wiki moja iliyopita.
SOMA : Waliokufa mafuriko Somalia wafikia 29
Mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi kutokana na mvua hiyo yamesababisha vifo vya watu 613 katika eneo hilo.