Hali tete ongezeko hali mbaya ya hewa

KAIMU Mkurugenzi Mkuu, TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Mabadiliko ya Sayansi ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dk Ladislaus Chang’a amesema bado hali ni tete duniani katika ongezeko la hali mbaya ya hewa.

Dk Chang’a amesema katika mwaka 2023 kumekuwa na ongezeko kubwa la joto kwa kiwango cha 1.4 ukilinganisha na miaka mingine.

Akizungumza leo Agosti 21, kwenye warsha yenye lengo la kujadili namna bora ya kufikisha taarifa kwa wananchi ya utabiri wa mvua za msimu wa vuli Oktoba hadi Desemba mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, ambayo ni Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, na Ukanda wa Ziwa Victoria.

Amesema taarifa za hali ya hewa ni muhimu katika kujipanga kwa kuendeleza shughuli za kiuchumi, hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka ndani ya miaka mitano utabiri au masuala ya tahadhali yawafikie watu wote duniani.

SOMA: TMA yatabiri mvua kanda ya ziwa

 

View this post on Instagram

 

A post shared by TMA (@tanzaniameteorological)

Akizungumzia suala la miundombinu, Dk Chang’a amefafanua kuwa Tanzania ni kati ya nchi iliyowekeza kwa kiwango kikubwa cha miundombinu ya hali ya hewa jambo lililosababisha kuwa wenyeji wa warsha itakayohusishwa wadau kutoka duniani.

Usahihi wa msimu wa mvua za masika ni asilimia 98.4 yote haya yakitajwa kusababishwa na miundombinu ya uhakika ambayo imewekezwa na Serikali ya Awamu ya Sita. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, inatarajia kutoa taarifa rasmi ya msimu wa mvua za vuli Agosti, 22 2024.

Habari Zifananazo

Back to top button