Halmashauri kutekeleza agizo la Waziri Mkuu

MKURUNGEZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Tatu Isike amesema halmashauri hiyo imejipanga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kutaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi na darasa la awali.

Akizungumza mkoani hapa, Isike amesema yupo kwenye mazungumzo na watendaji wa kata zote kwenye halmashauri kujadili na kupanga kwa pamoja namna bora ya kutekeleza agizo hilo.

Isike amesema hayo leo Julai 11 wakati akizungumza na watendaji wa baadhi za Kata katika Halmashauri ili kuwasikilza kwa karibu changamoto zao na namba bora ya kuboresha na kushirikiana kiutendaji.

“Moja ya vipaumbele vyetu watendaji wote ni kuhakikisha maagizo ya viongozi wetu yanatekelezwa kama ipasavyo na moja wapo ni kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na shule ya Msingi na darasa la awali,” amesema.

DED huyo amewataka wantendaji wa Halmashauri kuhakikisha kila mmoja anasimamia na kutekeleza majukumu ya kwa ufasaha zaidi ili kuleta matokeo chanya kwenye maendeleo ya Halmashauri hiyo.

Amesema serikali inatoa hela nyingi sana ikiwa na lengo njema kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki ikiwemo elimu kwa watoto.

Akiwa kwenye ziara ya kikazi Wilaya ya Mtwara, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitaka wakurungezi watendaji Halmashauri zote nchin kuhakikisha wanajenga shule za Msingi kwenye kila kijiji pamoja na darasa la awali ili kuwawezesha watoto kwenda shule kwa urahisi.

Aliwataka wakurungezi hao kushirikiana na mabaraza ya madiwani na maafisa elimu Msingi kuhakikisha agizo hilo linatekelezaka.

Majaliwa alisema kuwa na shule ya Msingi kila kijiji na darasa la awali ni mpango mkakati wa serikali kuboresha Mazingira ya kutolea elimu nchini.

 

Habari Zifananazo

Back to top button