Halmashauri zaelekezwa kuwapa mafuta wenye ualbino

​WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dk Festo Dugange amesema serikali imezielekeza halmashauri zote kutenga bajeti na kununua mafuta kinga ya watu wenye ualbino na kuyagawa kwa wahitaji.

Dk Dugange ametoa taarifa hiyo leo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha tano mkutano wa 14 wa Bunge la 12.

“ Serikali inatambua umuhimu wa kuwezesha upatikanaji wa mafuta kwa watu wenye ualbino kupitia halmashauri nchini.” Amesema Dk Dugange.

Advertisement

Amesema Katika mwaka wa fedha wa 2021/22 na 2022/23 jumla ya halmashauri 41 zilitenga na kununua mafuta kinga yenye thamani ya Sh milioni 47 na kuyagawa kwa wahitaji.