Halmashauri zatakiwa kutenga bajeti kuajiri watumishi wa afya

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga bajeti itokanayo na mapato ya ndani kuajiri watumishi wa afya wa mkataba.

Ummy alisema hayo jana alipofanya ziara wilayani Kishapu, na kupokea taarifa ya huduma za Afya wilayani humo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, Joseph Mkude.

Alisema tatizo la upungufu wa watumishi wa afya lipo maeneo mengi, sababu Wizara ya Afya haikuwa na kibali cha kuajiri kutoka kwa Rais,na kwamba mwaka huu ndiyo wamepata kibali, nakuagiza pia halmashauri zitenge mapato ya ndani kuajiri watumishi wa afya kwa mkataba.

Advertisement

“Naendelea kuhamasisha Halmashauri kutumia mapato ya ndani kuajiri Watumishi wa Sekta ya Afya kwa Mkataba ili kupunguza upungufu uliopo wa watumishi wa afya,”alisema Waziri Ummy.

Alisema pia Wizara hiyo ya Afya itazungumza na wadau wao mbalimbali wa maendeleo, wakiwamo Global fund na Taasisi ya Benjamini Mkapa,kuona namna ya kuwasaidia kuajiri watumishi wa afya kwa mkataba, wakati na wao wakiendelea kuajiri baada ya kupata kibali.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *