GAZA, PALESTINA: KUNDI la Hamas linatarajia kuwaachilia mateka wengine Jumamosi hii kama ilivyopangwa katika makubaliano ya usitishaji wa mapigano.
Hii ni kauli inayotoa matumaini ya kutatuliwa kwa mvutano mkubwa ambao ulikuwa ukitishia kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha vita.
Hamas imethibitisha dhamira yake ya kuendelea na mchakato wa kuwaachilia mateka wote wa Israel kulingana na ratiba iliyopangwa. SOMA: Israel, Hamas mambo safi
Wasuluhishi wa mgogoro huu, Misri na Qatar, wanaendelea kufanya kazi kuhakikisha vikwazo vyote vinaondolewa na makubaliano ya kusitisha vita yanaendelea kutekelezwa.
Hata hivyo, Hamas awali ilitishia kuchelewesha kuwaachilia mateka wa Israel kwa kuliishutumu Israel kwa kutotekeleza wajibu wake, ikiwemo kushindwa kuruhusu vifaa kuingia Gaza, jambo lililosababisha Israel kutoa tamko la kuendelea na mapigano.