Israel, Hamas mambo safi

ISRAEL: ISRAEL na kundi la wanamgambo wa Hamas wamekamilisha zoezi la tano la kubadilishana mateka wa Israel kwa wafungwa wa kipalestina kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miezi 12.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba Israel imewaondoa wanajeshi wake katika eneo la kimkakati la Netzarim lililopo Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amewaamuru wajumbe wa Israel kwenye mazungumzo ya amani kurejea nchini Qatar ili kujadili mpango wa kusitisha mapigano kati ya nchi yake na kundi la Hamas baada ya kukamilika awamu hiyo ya tano ya kubadilishana mateka wa Israel kwa wafungwa wa kipalestina.

Advertisement

Mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 2023 yalisababisha vifo vya watu 1,210 nchini Israel wengi wao wakiwa raia. Na katika hatua ya Israel ya kulipiza kisasi imesababisha vifo vya takriban watu 48,181 katika Ukanda wa Gaza.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *