Harris athibitisha matokeo ya urais bungeni

MAREKANI : MAKAMU wa Rais wa Marekani na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Demcratic, Kamala Harris, ameongoza shughuli ya bunge la nchi hiyo kuidhinisha ushindi wa Donald Trump, kuwa rais mpya.

Hapo jana, Bunge la Marekani lilifanikisha kwa wepesi tukio hilo kuthibitisha kwa njia za kidemokrasia kwa taifa hilo  bila ya  mashaka yoyote.

Makamu wa Rais Kamala Harris alisimamia zoezi hilo la kuhesabu kura za wajumbe na kisha akamtangaza rasmi aliyekuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi wa Novemba 9 kuwa ndiye mshindi halali.

Advertisement

“ Idadi kamili ya wajumbe walioteuliwa kumchagua rais wa Marekani ni 538. Ndani yake, wingi wa kura ni 270. Kura za rais, Donald J. Trump wa jimbo la Florida alipata  kura 312. Kamala D. Harris wa jimbo la Carlifornia alipata kura 226”.

SOMA:  Trump ashinda uchaguzi Marekani