MAREKANI : MGOMBEA wa Chama cha Republican nchini Marekani,Donald Trump ametangazwa kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani na kuahidi kuliponya taifa hilo.
Matokeo ya uchaguzi yamemuweka mgombea huyo wa Republican kifua mbele dhidi ya mgombea wa Demokratic Kamala Harris .
Akiwahutubia wafuasi wake mapema leo hata kabla ya vyombo vya habari kumtangaza mshindi, rais huyo wa zamani wa Marekani amesema ushindi huo haujawahi kutokea katika historia ya Marekani.
“Ahsanteni sana inapendeza tuna maelfu ya marafiki kwenye vuguvugu letu hili, hili ni vuguvugu halijawahi kushuhudiwa”, alisema Trump.
Katika uchaguzi huo, Trump amepata kura nyingi katika majimbo makubwa matatu ambayo yanadaiwa kuwa yanamaamuzi ikiwemo Pennsylvania, Georgia na North Carolina.
Ushindi wa Trump umekifanya Chama cha Republican kupata nafasi nyingi katika baraza la seneti ukilinganisha na kura zilizopigwa kwa Chama cha Demokratic.
Hivi sasa viongozi mbalimbali duniani wameendelea kutoa salamu za pongezi kwa Trump akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na viongozi wa madola makubwa ya Ulaya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte.
SOMA: Uchaguzi Marekani hautabiriki – Watafiti
Comments are closed.