MAREKANI : WAMAREKANI bado wanaendelea kupiga kura kwa njia tofauti kuchagua mgombea wa urais wa Marekani atakayestahili kuingia Ikulu ya White House katika uchaguzi unaoambiwa usioweza kutabirika.
Kamala Harris ni mgombea wa chama cha Democratic ambaye pia makamu wa rais na Trump ni mgombea wa chama cha Republican anayetafuta muhula wa pili wa miaka minne ijayo.
Katika wiki za lala salama za kampeni zao, wagombea hawa walizunguka kupiga kampeni katika majimbo 7 muhimu yanayodaiwa kuwa ndiyo yatakayoamua mshindi wa uchaguzi huo.
Hatahivyo, watafiti mbalimbali wa kura za maoni wamesema kati ya wagombea hao hakuna mgombea yeyote ambaye ana uongozi mkubwa katika majimbo ya Pennsylvania, Michigan, Wisconsin, georgia, North Carolina, Nevada na Arizona.
” kuna uwezekano mkubwa kwa mgombea yeyote yule kushinda katika majimbo haya yenye ushindani na ushawishi mkubwa wa kuchagua”, walisema.
Comments are closed.