Harris Trump wafungana matokeo

MAREKANI : MATOKEO ya kwanza ya uchaguzi wa Marekani yametangazwa katika kijiji kidogo cha Dixville Notch huko New Hampshire ambapo wagombea wote wawili wa urais Kamala Harris na Donald Trump wamefungana kwa kura.

Mgombea wa Democratic Harris amepata kura 3 sawa na mwenzake wa Republican Trump alipata kura 3.

Kijiji hicho kilicho karibu na mpaka wa Canada kimeshuhudia kufungwa vituo vya kupigia kura  saa sita  usiku .

Advertisement

Kijiji cha Dixville Notch kimekuwa na utamaduni wa kufungua vituo vya upigaji kura usiku tangu mwaka 1960.

Kwa kuwa wapiga kura waliojiandikisha walikuwa sita pekee, zoezi la kuhesabu kura lilifanyika kwa  haraka.

SOMA: Trump akana kubatilisha matokeo uchaguzi 2020

1 comments

Comments are closed.