Hati za ardhi 283 zatolewa siku tatu Ubungo

DAR ES SALAAM; IKIWA ni siku tatu tangu kuzinduliwa kwa utoaji wa hatimilki za ardhi kupitia programu ya Ardhi Kliniki Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, hati 283 zimeshatolewa na migogoro ya ardhi 69 imetatuliwa.

Mratibu  wa programu hiyo ya urasimishaji katika Manispaa ya Ubungo, John Ilomo ameeleza hayo alipokuwa akizungumzia muitikio wa wananchi kuchukua hati zao.

“Mpaka sasa tumefanikiwa kutoa hati hizi hii inaonesha kuwa wananchi wameelewa na wameitikia  wito kufika kwenye viwanja hivi kwa ajili ya kujipatia hati, hakika wananchi wameelewa kuwa serikali imewasogeze huduma,” amesema.

Advertisement

Amesema japokuwa kuna hali ya mvua, lakini mwitiko wa wananchi umekuwa mzuri wanajitokeza hali inayoonesha kuwa walikuwa na uhitaji wa huduma hiyo karibu. Lengo la manispaa ya Ubungo ni kutoa hati 3419 kwa wakazi wake.

Katika hatua nyingine, wanandoa wametakiwa kujitokeza kwa ajili ya kupata huduma ya kumiliki ardhi kwa pamoja, kwa kuwa ipo kisheria.

Paul Kitosi kutoka Timu ya Uratibu Mradi Uboreshaji Salama wa Milki za Ardhi, amesema hayo wakati wa utoaji wa hati katika Halmashauri ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.

“Sheria zinaruhusu kumiliki ardhi mama na baba. Hii ni fursa kwa sababu wengi hawajui kama anaweza kumiliki yeye na mke wake. Tunahimiza kwa sababu tunaona ni fursa,” amesema.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *