Hatma ya Afrika kuhusu nishaiti kuamuliwa Tanzania

DAR ES SALAAM: AZIMIO la kuwaunganishia umeme Waafrika milioni 300 linatarajiwa kusainiwa nchini kwenye Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika ‘Mission 300’ unaoendelea leo na kesho Januari 28 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Nchi 24 ambazo Wakuu wa Nchi zao wamethibitisha kushiriki ni Algeria, Comoro, Liberia, Lesotho, Botswana, Kenya, Ghana, Gabon, Sierra Leone, Ethiopia, Sudan, Malawi, Zambia, Somalia, Guine Bisau, Burundi, Mauritania, Kongo Brazzaville, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Libya, Nigeria, Djibouti na Gabon.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema Wakuu wa Nchi, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Naibu Mawaziri Wakuu wamethibitisha kuhudhuria kwenye Mkutano wa Mission 300

Advertisement

“Tulipokea Wakuu wa Nchi 19 wakati wa Kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999 na Wakuu wa Nchi 15. Wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mwaka 2019, mkiangalia idadi ya Wakuu wa Nchi katika mkutano huu ni kubwa ukilinganisha na matukio hayo mawili yaliyopita,” Balozi Kombo amesema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *